CUF yakanusha kadi kurudishwa

  •  

    Hivi karibuni kumekuwa na taarifa za uongo na propaganda zinazoenezwa na Hamadi Rashid kwenye vyombo vya habari kwamba zaidi ya wanachama 1000 wa CUF wa mikoa ya Dar es Salaam na maeneo mengine wamerudisha kadi na kumkabidhi Hamad Rashid.

     

    CUF imefuatilia na kubaini habari hizi ni za uongo na chama kimebaini kwamba kadi anazoonesha kwa waandishi wa habari si za wanachama bali ni za kutengenezwa ambazo aliziandaa wakati wa Kura za mao ni za kuwapata wagombea wa Ubunge na kilishi kwa uchaguzi Mkuu wa mwaka 2010 na Chama kuzuia uingizaji wa wanachama wapya muda mfupi kabla ya kura za maoni.

     

    Kwa wakati huo Hamadi alikuwa ameandaa Kadi mpya 7000 ziweze kumsaidia katika kinyang’anyiro hicho, hivyo basi hakuna wanachama 1000 waliompelekea kadi kwani wanaCUF wako ngangari na chama kipo imara kwa kuwa wanatambua kuwa wao si wanachama wa UHS (United Hamad Suppoters), bali wao wanachama wa The Civic United Front hivyo hawapo kwa maslahi ya mtu binafsi.

     

    Chama cha wanachi CUF kinatoa tahadhari kwa wanachama wake kwamba kumekuwa na zoezi la kununua kadi za wanchama wa CUF  na Hamad kwa kutumia watu mbalimbali,Hivyo mwanachama yoyote asikubali kutoa kadi yake kwa namna yoyote na kwa mtu yeyote.

     

    Katika hatua nyingine chama cha wanachi CUF kitakuwa na mkutano mkubwa wa hadhara  katika viwanja vya Barafu-Manzese kuanzia saa 7 mchana kesho jumamosi tarehe 7Januari 2012.

     

    Mkutano huo wa hadhara ambao utahutubiwa  na Katibu Mkuu wa Chama cha Wananchi CUF na Makamu wa kwanza wa serikali ya Mapinduzi  Zanzibar Mh.Maalim Seif Sharif Hamad  utahudhuriwa pia na viongozi wote wa CUF taifa isipokuwa Mwenyekiti Taifa Prof.Lipumba ambaye yuko Marekani kwa kazi za kimataifa.

    Mkutano huo utakuwa unatoa ufafanuzi wa kina juu ya maamuzi ya Baraza Kuu la Uongozi la Taifayaliyofikiwa katika kikao chake kilichoketi hivi karibuni Mjini Zanzibar pamoja na kuelezea mustakabali wa chama na hali ya umaskini unaoikabili nchi kwa ujumla.

    HAKI SAWA KWA WOTE

    IMETOLEWA NA AMINA MWIDAU

    MKURUGENZI WA HAKI ZA BINADAMU NA UENEZI

Comments

0 comments