
Waziri wa Habari na Utamaduni, Mh. Emmanuel Nchimbi akishirikiana na Mnadhimu Mkuu wa Upinzani Bungeni, Mh. Tundu Lissu wamewapatanisha mahasimu wawili Mbunge wa Mbeya Mjini, Mh. Joseph Mbilinyi na Mkurugenzi wa Clouds Media Ruge Mutahaba. Katika usuluhishi huo, pande zote mbili zimekubaliana kuweka pembeni tofauti zao na kuzizika kabisa kwa maslahi ya wafuasi wao.
Nchimbi amemaliza ugomvi huo ambao umedumu kwa takribani miaka mitatu baana ya kufanya vikao kadhaa na wawili hao na hatimaye kusaini mkataba wa kumaliza tofauti zao zilizokuwepo hao kabla..Akizungumza na wandishi wa habari hii leo Nchimbi amesema ugomvi mkubwa uliokuwa unawahusu wawili hao ni kuhusiana na masuala ya maslahi na haki za wasanii ambapo sasa wameamua kuachana nao na kuendelea na shughuli zao.
Amesema miongoni mwa mambo waliyokubaliana ni kumaliza mgogoro n uhasama baina yao, wanashirikiana kufanikisha haki na jitihada ya kuinua maslahi ya wasanii, kufanya jitihada ya pamoja ya kuunganisha vyama vya wasaniivya TUMA na TFU ili kutetea maslahi ya wasanii wakiwa na umoja zaidi. Nchimbi amesema suala la mwisho ambalo wawili hao pia wamekubaliana ni watu wote wanaowaunga mkono katika mgogoro waliokuwa nao wamalize uhasama na kufungua ukurasa mpya na ushirikiano baina yao.
=================================
Maneno ya Sugu mwenyewe.
Kwanza poleni na samahanini kwa hali ya sintofahamu iliyotokea leo kutokana na taarifa za ghafla za usuluhishi kati yetu na Ruge/Clouds FM, ni kutokana na unyeti wa issue yenyewe ilibidi tufanye hivyo kwa nia njema kabisa...
Kwanzanaomba tujipongeze kwa kuwa tukio la leo ni ushindi kwa Vinega kwa maana kwamba madai yetu yote ya msingi ndio yalikuwa msingi wa majadiliano na Ruge amekubali kuyatekeleza yote...
Kuanzia suala la studio ya Rais kurudishwa kwa BASATA ili iwe ya wasanii wote, pia TFU ijikabidhi kwa chama halali cha wasanii yaani T.U.M.A kama ambavyo tulikuwa tunadai na mpaka issue za wasanii kunyanyaswa na kubaniwa na pia suala la malipo hafifu vyote vimejadiliwa na kukubaliwa kwa utekelezaji...
Haikuwa kazi rahisi, kwanza ilianza kwa wao kumpigia Mwenyekiti wangu Mbowe kutaka tukae chini, ambapo Kamanda Mbowe alinishauri tukae nao chinikamakweli wana nia ya kuyamaliza...
Baadaye wakampigia Mr Shigongo ambaye ni wazi kuwa ni kati ya watu wangu wa karibu naye baada ya kuongea na Mr. Kusaga tu alinipigia na kunishauri hivyo hivyo...
Nakamahaikutosha wakalifikisha hili suala kwenye Kamati ya Bunge ambayo ilinitaka niipe maelezo ya kiini cha mgogoro na nikafanya hivyo ambapo pia baada ya kunielewa wakashauri nikae nao chini... Na hatimaye suala hili likaishia mikononi mwa Waziri Nchimbi pamoja na Mhe. Tundu Lissu(MP) kuwa wapatanishi wetu...
Waziri Nchimbi akaanza kwa kumuita Ruge Dodoma na alikuja tukakaa kwa hatua ya kwanza na hatimaye leo tukakaa tena makao makuu ya Wizara ya Utamaduni chini ya Dr Nchimbi na Mhe Tundu Lissu na hatimaye tukafikia hatua hii ya leo...vita yetu ilikuwa na hoja hatukuwa tunapigana tu kwa chuki binafsi kama baadhi ya watu walivyokuwa wanajaribu kuiweka, kwa hiyo kama hoja zetu zimeeleweka kwa sasa tunatakiwa kushukuru na kufurahia...
Lakini naomba niwahakikishie misimamo iko pale pale na nimewaweka wazi kuwa anti-virus itaendelea kuwepo ili kuendelea ku-scan virus wenginekamamameneja masoko na wengine watakaojitokeza kwani nchi inaposhinda vita au hata kufikia tu makubaliano ya amani na nchi adui yake haina maana nchi hiyo inavunja jeshi lake...
Asanteni sana...
Picha zaidi: http://bongoline.com/albums/view/586
Comments